Social Icons

Wednesday, February 15, 2017

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUPIMA AFYA BURE JUMAMOSIMkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa (wa kwanza kulia) akitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushiriki  katika Tamasha la Mazoezi ambalo limepangwa kufanyika Jumamosi ijayo Februari 18 kwenye viwanja vya Leaders  Club , Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo litawapa wananchi fursa ya kufanya mazoezi na kupima afya bure  ikiwa ni katika kuitikia wito wa Makamu wa Rais nchini Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
Aidha Tamasha hilo limepangwa kuanza saa 12 asubuhi  hadi saa saba mchana  . Huku likilenga  kuhamasisha wananchi  kufanya mazoezi.

No comments:

 
 
Blogger Templates