Social Icons

Saturday, September 24, 2016

TSN YADHAMINI MECHI KUCHANGIA WAATHIRIKATETEMEKO LA ARDHI BUKOBAMkuu wa  kitengo cha Masoko na Biashara TSN , Jahu  Mohammed Kessy  akiwakabidhi  wasanii  jezi kwa ajili ya  mechi ya kuchangia  maafa ya tetemeko la ardhi  Bukoba.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara Jahu Mohamed Kessy, amesema TSN imejitokeza kudhamini mechi hiyo itayofanyika uwanja wa taifa, jumaapili tarehe 25 september, na hivyo kuwataka wananchi, mashirika na kampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa Kagera waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo la ardhi.


Alisema wao kama TSN wameguswa na janga hili na hivyo mbali na michango yao mingine ya moja kwa moja wameona umuhimu wa kushirikiana na wasanii wa bongo fleva na bongo movie kuhamasisha uchangiaji huo kwa pamoja ilikuweza kuwashirikisha na wengine.

“TSN, Tanzania sisi Nyumbani, tunaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti  kwa lengo la kuhamashisha uchangiaji wa pamoja,”

Alisema mechi hiyo inatazamiwa kuchezwa saa tisa mchana katika uwanja huo wa Taifa.

No comments:

 
 
Blogger Templates