Social Icons

Thursday, August 25, 2016

WASANII WAUNGANA KUPINGA MAANDAMANO YA UKUTA

 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wasanii wapenda Amani nchini, Asha Baraka akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tamko lao la kuungana pamoja kupinga Maandamano ya UKUTA, Septemba 1.  
Mwenyekiti wa Umoja huo, Steven Mengere (Steve Nyerere) akizungumza juu ya kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika  Septemba Mosi kote nchini.
Mwanamziki na Malkia wa Nyimbo za Taarab, Khadija Kopa akizungumza katika mkuatano wa Kupinga maandamano ya UKUTA jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Ally Choki akizungumza katika Mkutano wa Kupinga maandamano ya UKUTA jijini Dar es Salaam leo.

WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba 1,mwaka huu.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere amesema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.

"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere

Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka amesema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.

Amesema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.

Hatahivyo ameomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele. 

No comments:

 
 
Blogger Templates