Social Icons

Monday, May 23, 2016

WAZIRI NAPE AZINDUA MFUMO WA KISASA WA WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Picha na Geofrey Adroph(Pamoja Blog)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.
Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile, Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION
Meneja wa Biashara wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo 
Munalove(kushoto) akimwelekeza mama mzazi wa Wema Sepetu jinsi ya kujiunga na WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mara bada ya kufanyika kwa uzinduzi huo
Msaniii wa Bongo Movie, Wema Sepetu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye baada ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini
Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wake wa huduma ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION
Wema Sepetu akiwa amemkumbatia mama yake mzazi mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi



Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye amesema kwamba  serikali itakuwa pamoja na msanii nyota Wema Sepetu katika kila hatua ili kuhakikisha mwaba anapata haki zake  bila kudhulumiwa.
Nnauye alisema hayo jana jioni kwenye uzinduzi wa  mfumo wa kisasa kabisa wa msanii huyo nyota wa filamu nchini itakayofahamika ,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

 Wema almaarufu kama  'Maadam'  alisema  ya waandishi wa habari   kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali  yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.

Wema Sepetu alisema kuwa huu ni mwanzo mzuri na aliahidi kutumia huduma hiyo kutoa elimu kunufaisha jamii,kutangaza sanaa na utamaduni wetu,kuwa karibu na wapenzi ama mashabiki wake wote watakaokuwa wanahitaji kupata habari zake za kweli na uhakika.

Mfumo huu na wa kipekee kabisa kwa mwanadada huyo,umezinduliwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi .

Mfumo huu  ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote."Mfumo wangu huu ni wa kipekee na wa kwanza katika Afrika Mashariki kwa msanii wa tasnia ya Filamu,mfumo huu utaleta fursa nyingi sana zikiwemo ajira kwa vijana na wasanii wenzangu na kutambulika kirahisi"alisema Wema Sepetu.

Kujua mafanikio na Umuhimu wa kazi za Usanii Tanzania,huduma ya Wema Sepetu Mobile ni rahisi na ya uhakika,unatuma neno WEMA kwenda 15404 kwa makato ya sh. 60 tu  na   unaunganishwa  na kuaanza kupokea taarifa na habari za Wema sepetu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno,picha na video kutegemeana na aina ya simu yako unayotumia.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye amempongeza  Wema  kwa kubuni mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote na pia utamsaidia kumuingizia kipato na kuweza kuisaidia jamii inayomzunguka kwa namna moja ama nyingine na kuahidi kuwa serikali itamsaidia ili kuhakikisha sasa anapata haki zake ambazo alizipoteza kuho nyuma.
"Inasikitisha tumeona vyombo vingi vya habari vikijinufaisha  binafsi kwa zaidi ya miaka kumi sasa  na kutengeneza fedha nyingi huku Wema akiwa hana kitu sasa basi nimesimama hapa kwa niaba ya serikali naahidi  haki yako haitapotea na utanufaika kutokana na jina lako wale ambao walikuwa wakitumia  jina lako na kuandika mambo yasiyokuwa na ukweli mwisho wao umefika" alisema Nnauye


 Wakati huohuo Meneja wa Biashara  wa Hartmann Trader ambao ndiyo watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina aliweza kufafanua  namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujiunga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo ambayo itapatikana kwenye simu za aina zote .

No comments:

 
 
Blogger Templates