Social Icons

Monday, August 31, 2015

CCM JIMBO LA KAWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU YAMNADI KIPPI WARIOBA

Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana. PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiinadi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
MAMA MZAA CHEMA … Mama Evelyne Warioba ambaye ni mama mzazi wa Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Mhamasishaji maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo. 
MANISPAA  ya Kinondoni imetenga  fedha kiasi cha Sh. Bil.1 ambazo zitagawiwa katika kata  kumi kwa ajili ya mikopo isiyokuwa na masharti kwa vijana.

Hayo yalisemwa na  Mtashiki Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda  alipokuwa akimnadi  mgombea wa Ubunge Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Kippi Warioba kwenye viwanja vya Boko CCM Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kwa kusema kuwa tayari Manispaa imetenga kiasi cha Sh.Bil. 1 kwa jimbo la Kawe ambapo kila kata itapata Sh. Mil.100  ambazo zitatolewa mikopo bila masharti kwa vijana.

Mwenda aliongeza kwa kusema kwamba fedha hizo ambazo zimetolewa na CCM ni mwendelezo kwa  kuwawezesha vijana na  kwa katika kipindi kilichopita walitoa mikopo  bila masharti kwa vijana yenye thamani ya Sh.Mil 500.
 “Endapo mtachagua  wagombea wa CCM  itakuwa ni  kazi rahisi  kwa serikali yetu ijayo itakayokuwa chini ya Rais Magufuli  wote kwa pamoja wataweza kukaa na kuzungumza namna ya kumalizia ujenzi wa Hospitali ya Mabwepande na maendeleo mengine mengi tu yatakuja endapo mtamchagua Warioba” alisema.

Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kuwa kwa kipindi kilichopitita CCM haikuwa na Mbunge wa Kawe lakini serikali  kwa kupitia Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kutatua migogoro mingi ya ardhi  ikiwemo wakazi wa eneo la Chasimba ambao hivi  karibuni watapewa haki ya kumiliki ardhi  hiyo kwa kila mmoja  kupatiwa hati miliki.

Mwenda aliongeza kwa kusema kwamba CCM hawatakubali kupoteza nguvu za maendeleo waliyoyaanzisha  huku akiwasisitiza wakazi wa Kawe waichague CCM kuanzia madiwani , mbunge na rais ambaye ni John Magufuli.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Warioba alisema kwamba atazingatia suala zima la migogoro ya ardhi Kinondoni  na kwa wakazi wa Kawe.

“Nitakaa na wadau wote wa Kawe kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwani nayajua matatizo yenu yote, nayafahamu matatizo ya Jimbo la Kawe kwa ujumla” alisema Warioba.

Aliongeza kwa kusema kwamba atahakikisha anatatua tatizo la ukosefu wa matundu ya vyoo katika shule za Kawe hivyo atakuwa na vikao vingi katika kila kata kuwasikiliza na kuweka mikakati ya kurudisha jimbo hilo CCM kwani hivi sasa linashikiliwa na Halima Mdee Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema).


Aidha Warioba alitumia muda wake kuwaombea kura madiwani kumi wa Kawe ambao wanawania nafasi hiyo kwa kusema kuwa ili aweze kufanya kazi vizuri anaomba wananchi wachague madiwani wa CCM, Mbunge CCM na Rais wamchague  wa  CCM ambaye ni John Magufuli.

No comments:

 
 
Blogger Templates