Social Icons

Saturday, August 25, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAZINDULIWA MKOANI KILIMANJARO

 Usiku wa Ijumaa utabaki kukumbukwa kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na uzinduzi wa aina yake wa tamasha la 11 la Serengeti Fiesta lillilofana mkoani hapa.

Tanzania Daima ambayo ilikuwepo katika eneo la tukio hilo ilishuhudia mamia ya vijana wakiwa wamejitokea kwa wingi katika uzinduzi huo wa aina yake.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama aliwahamasisha mamia ya mashabiki na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi huouliofanyika katika Viwanja vya Chuo Cha Ushirika kushrehekea kwa amani na utulivu pamoja na kutosahau kujitokeza katika zoezi la sensa.

Baaadhi ya wasanii waliofunika katika uzinduzi huo ni Shetta , Richie Mavoco, Makomando, Linah, Joh Makini, Mwana Fa bila ya kumsaha mwanamuziki wa kimataifa ambaye pia alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Big Brother 2012 Prezzo kutoka nchini kenya.

Wakati huohuo uzinduzi huo ulinogeshwa nawasanii wa nyota wa filamu nchini ambao ni Aunt Ezekiel, Ray Kigosi ‘Ray’, Mwenyekiti wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’, Steve Nyerere na Wema Sepetu ambao walikuwepo katika uzinduzi wakiwa ambapo walikuwa katika msafara huo kwa minajili ya kusaka vipaji vya kucheza filamu kwa wakaazi wa mkoani hapa.Wasanii hao ambao walitambulishwa jukwaani

Pia waliweza kuonesha namna wanavyoweza kunengua mbali ya kucheza filamu huku mashabiki wakimpigia kelele Wema atingishe nyonga zake mara kadhaa nay eye alifanya hivyo na kushangiliwa ipasavyo.

Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Prime Time Promotions ambayo ni Kampuni dada na Clouds Media Group yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.

Wasanii wengine walio onesha uwezo wao katika uzinduzi huo ni pamoja na Juma Kassim ‘Nature’, Ferooz, Stamina, Tash &Juru, Mr. Nice, Recho, Jambo Squard, Rich Mavocal, Ommy Dimpoz, Godzilla na Bob Junior. Jumapili usiku  Agosti 26 tamasha hili litarindima ndani ya uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.

No comments:

 
 
Blogger Templates