Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la Bomoa bomoa nyumba zilizojengwa maeneo ua Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam jana Mei 17, 2012. Katika picha kutoka (kushoto) ni Katibu wa Wizara ya Ardhi, Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, baada ya mazungumzo hayo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
RAIS SAMIA ATOA POLE KWA WAATHIRIKA WA AJALI YA KUDONDOKEWA NA GHOROFA
KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
1 hour ago
0 Comments