Social Icons

Friday, February 3, 2012

MAIMATHA JESSE SEND OFF PARTY ILIYOFANYIKA USIKU WA JANA FEB02 2012 DIAMOND JUBILEE VIP HALL

 Maimathan Jesse ambaye ni Mtangazaji machachari wa Luninga hasa vipindi vya muziki wa dansi nchini jana aliweza kutimiza njozi yake katika shughuli yake ya Send Off , iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP jijini Dar es Salaam .

Hapa  akifurahi mara baada ya kufika katika meza ya baadhi ya mashosti  waliofika kujumuika naye  jana usiku.Kwa raha zako bibi wala hugombwi  tena wala usiwajali waosha vinywa  ambao kucha kutwa hawalali kufuatilia ya wenzao semeni sasa Kimwana ndo huyoo kesha patawake.Mpendwa Mai nakutakia maisha yenye kheri,baraka amani , upendo  tele vicheko na ucheshi wako utawale ndani ya nyumba yako.
 Chekaa kwa raha zako Mummy  tena wala usiwajali visokorokwinyo waliojaaliwa mitinanyongo.
 Hapa bi harusi Maimatha akisalimia katika meza ya mashosti kwa mbwembwe na ucheshi wake kama jinsi alivyo kabla haja badili nguo na kwenda mfichua  mume wake.
 Hapa ni katika miondoko ya inuka wakuone mpenzi wangu eee ooh ooh ooh ,isome kimya kimya hahaaa Mai poteza mbayaa
 Mcheza Filamu nyota  wa Bongo Movie Aunt Ezekiel naye alikuwa kati ya wakina dada waliompasapoti Maimatha.
 Alanisa Khadija Omar Kopa alikuwepo hapa akifanya mambo yake mbele ya Asha Baraka.
 Salma Dakota  Mtangazaji kituo cha Redio One  akipozi kwa picha.
Kama kawaida hatukulala jana hapa mara baada ya kuwasili Diamond Jubilee kuhudhuria shughuli kwa raha zetu sema tenaaaa hahaaa. 
 Kutoka kulia ni Khadija mhangaikaji wa Blogu ya Bongoweekend, Khanifa Hamidu Mtangazaji  na Salma Dakota wote ni watangazaji wa  Redio One ndani ya ukumbi.Hii inaitwa ng'aring'ari. 
 Mamaa wa Yaliyomo Yamoo Lady Hanny cheka wakuonee mamaaa.
 Stori zikiendelea, kusogoa imo jamani  ati tena hapa mimi ndiyo nikuwa mwenyekiti wa kustorisha..
Acha tucheke na tufurahi  siye  waliochanganyikiwa na ugumu wa maisha na wanaoendekeza kununia watu na kuweka chuki  za hovyohovyo shauri zaoooo. 
 
Na hawa nao walikuwepo , mwenye bluu ni Baby Tall,Asha Said  'Sharapova' Maria Soloma na Dada lao Luiza Mbutu.

No comments:

 
 
Blogger Templates