Social Icons

Friday, September 16, 2011

KAMPUNI YA BIA SERENGETI KUTUMIA SH.MIL352 KATIKA KAMPENI YA KUNYWA POMBE KWA STAHA

 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha akiwa  katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni kabambe  iliyodhamiria  kuwatahadharisha  watu juu ya matumizi  sahihi  ya pombe katika kampeni hito SBL,imetenga  Sh. Mil.352 kwa  mwaka 2011/12 kujaribu  ujumbe  unaohamasisha  watu kubadili tabia zao juu ya unywaji wa pombe.Kulia ni Kamanda wa  Kikosi Cha Usalama Barabarani Mohammed Mpinga.
 WAZIRI wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha jana ameushangaa uongozi wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL), kwa kuanzisha kampeni ya kunywa pombe kwa ustaarabu huku akijiuliza watapata wapi faida endapo wanahamasisha unywaji wenye staha.
                        

Na Mwandishi Wetu

Aidha Vuai alitoa pongezi kwa SBL kwa kuanzisha kampeni hiyo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya unywaji wa staha itakayoenezwa nchi nzima.

“Nimefurahi kualikwa kuwa mgeni rasmi katikia uzinduzi wa kampeni hii, na nawapongeza SBL kwa kutambua ukweli kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi una madhara makubwa katika jamii na natoa wito kwa makampuni mengine yanayotengeneza pombe kuanzisha kampeni kama hii”, alisema Nahodha.

Nahodha alisema kuwa unywaji pombe kupindukia unasababisha hasara kubwa kwa mnywaji binafsi na kwa jamii ikiwemo ajali, vifo, umaskini na maafa mengine mengi.

Nahodha alifafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu za utafiti za 2007, ulevi umekuwa ukilisababishia taifa hasara kubwa ya asilimia 3.4% ya pato lake na kusistiza kuwa ajali zinazotokea kutokana na ulevi zimefikia asilimia 76.4.

Katika kuhakikisha udhibiti wa ajali hizo, Nahodha aliwataka makamanda wote wa usalama barabarani kuyakagua magari yote na madereva wanaoingia katika mikoa yao ili kuwabaini madereva wanaoendesha wakiwa wamelewa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL , Teddy Mapunda aliesema kuwa wametenga kiasi cha sh. Mil.352 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2012 katika kuitangaza kampeni hiyo nchi nzima na kwamba fedha hizo zitatumika katika kusambaza ujumbe wa kuhamasisha watu kubadili tabia zao juu ya unywaji wa pombe.

“Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika kwa kuwataka kuelewa hatari ya unywaji pombe kupindukia na kuwawezesha kufanya maamuzi kwa faida zao, maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.”

Alisema kuwa vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi na waathirikika wakubwa ni watu ambao hawahusiki kabisa na ulevi.

“Tutafanya kampeni hii kwa kutumia njia mbalimbali zitakazofikisha ujumbe kwa jamii ambazo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa baa, kuweka matanzagazo katika vyombo vyote vya habari, mabango barabarani, mafunzo kwa wanahabari, kuweka ujumbe katika bidhaa zetu, na tutafanya mihadhara kwa vijana wenye umri chini ya 18”, alisema.Mapunda alisisitiza kuwa utumiaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa wanywaji na jamii yote na ni kitisho kwa mustakabali wa taifa zima, na kwamba kampeni waliyoizindua itasaidia kuleta mabadiliko na ustawi wa taifa letu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Shamsi Vuai Nahodha akipokea vifaa maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Richard Wells, vifaa hivyo vitakavyotumika nchini kote ili kuwapima madereva wanaolewa huku wakiendesha magari.
 Aliyeinama kushoto ni Mkurugenzi  wa Mahusiano SBL, Teddy Mapunda  sambamba  Mkurugeni Mtendaji wa SBL , Richard Wells. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa SBL , Richard Wells akimpa mkono wa shukran Waziri Vuai mara baada ya kuzindua rasmi kapmeni ya unywaji wa staha.
 Baadhi ya washika dau wa Kampuni ya SBL,wakimsikiliza Waziri Vuai  katika uzinduzi ulifanyika katika hoteli ya Movenpic Dar es Salaa. 
 Mkurugenzi Masoko wa SBL , Ephraim Mafuru akitilia mkazo kampeni hiyo ya unywaji wa staha.
Aliyekaa katikati ni Meneja wa Bia ya Tusker Rita Mchaki akiwa na wafanyakazi wenzake wa SBL.
 MASHOSTITOOZZZZZZZZ.
Mhariri wa Habari za Michezo na Burudani Grace Hoka, katikati Moody Bawazir Mdau  na Mhariri wa Habari za Michezo  na Burudani Gazeti la Majira Suleiman Mbuguni wakiwa nje ya ukumbi mara baada ya uzinduzi.
 Somoe Ng'itu wa kwanza kushoto (Nipashe), Grace Hoka (Bingwa), Moody Bawazir Mdau na Suleiman Mbuguni (Majira) wakishoo love mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya unywaji wa staha.

No comments:

 
 
Blogger Templates