Social Icons

Saturday, May 14, 2011

WAZIRI NCHIMBI KUKUTABA NA WASANII WOTE.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Emmanuel
Nchimbi (Mb), atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia
tarehe 17 Mei na tarehe 18 Mei, 2011.

Waziri ataongea na wasanii kwa utaratibu ufuatao:-

17/05/2011 (Jumanne) Saa 4:00 asubuhi
• Wasanii Wote wa Sanaa za Muziki

18/05/2011 (Jumatano) Saa 4:00 asubuhi
• Wasanii Wote wa Sanaa za Ufundi, Filamu na Maonyesho

Izingatiwe kwamba Waziri ataongea na wasanii wa muziki wa aina zote
wakiwemo wa Kizazi kipya, Bendi, Disco, Asili, Taarab na kadhalika katika
siku ya kwanza. Katika siku ya pili yaani Tarehe 18/05/2011 ataongea na
wasanii wa Sanaa za Filamu, Maonyesho na Ufundi pekee.

Wasanii Wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi.

Lengo kuu la mikutano hii kati ya Waziri na Wasanii ni kuongelea
maendeleo ya fani za sanaa.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

No comments:

 
 
Blogger Templates