Social Icons

Monday, May 16, 2011

ISHA MASHAUZI ATOA KALI ASUSA KUIMBA KISA MDOGOWAKE HAKUING'ARA MISS DAR CITY CENTRE



KATIKA hali ambayo haikutegemewa na mashabiki mwishoni mwa juma Ijumaa iliyopita muimbaji anayechipukia kutoka katika kundi la Jahazi Taarab Isha Ramadhan Makongoro almaarufu kwa jina la 'Isha Mashauzi' pia mwenyewe anajiita Jike la Simba aligoma kupanda jukwani kutumbuiza kama ilivyokuwa imepangwa kisa eti mdogo wake hakuweza kupata sifa za urembo hivyo hakupenya hata katika kumi bora hivyo alichokifanya Isha ni kumchukua mdogo wake ambaye ilisemekana kwamba udugu wao ni toka nitoke na kumtia kwenye gari kisha kutokomea bila ya kujali kwamba yeye alikuwa ni msanii na alitakiwa awajibike katika kutoa burudani kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa kituo cha Miss Dar City Centre 2011.

No comments:

 
 
Blogger Templates