Social Icons

Friday, October 15, 2010

WAREMBO WA DUNIA WACHUANA KATIKA VAZI LA UFUKWENIBaadhi ya washiriki ambao ni warembo kutoka katika mataifa mbalimbali duniani wakiwa katika shindano la vazi la ufukweni, shindano hilo ni moja kati ya mataji madogo maadogo yanayoshindaniwa katika shindano hilo hilo la kumsaka mrembo wa dunia. Warembo hao wameanza kambi katika kisiwa cha Sanya nchini China ambako wanaendelea na maandalizi hadi kufikia fainali za shindano hilo zilizopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Tanzania inawakilishwa na mrembo wake Genevieve Emmanuel Mpangala ambaye anasema kuwa anafurahia kuwepo huko ikiwa ni pamoja na kujifunza mambo mbalimbali hiyo ni kwa mujibu wa barua pepe aliyotuma mara baada ya kuwasili Sanya.

No comments:

 
 
Blogger Templates