Social Icons

Friday, September 24, 2010

Msindi wa Pili BSS Atajwa Tusker Project Fame 2010

Peter Msechu mwenye miwani ambaye alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Bongo Star Search(BSS) hapa akiwa katika usaili hoteli ya Peacock Dar es Salaam Septemba 18,ambapo yeye yuko miongoni mwa washiriki 5 watakaoshiriki katika kinyang'anyiro cha Tusker Project Fame.Meneja Uhusiano na Habari wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda kwa kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager, ametangaza rasmi majina matano ya washiriki aliochaguliwa kuingia katika shindano la Tusker Project Fame 2010. Mapunda amesema mbali na aliyekuwa mshindi wa pili katika shindano la Bongo Star Search Peter Msechu wengine ni Janeth Audax, Christopher, Aneth Kushaba, Leah Mwambongela na Cynthia Bavo.Alisema washirki hao wataingia kambini leo pia mshindi katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha sh milioni 95 pamoja na kurekodi nyimbo katika studio ya kisasa nchini Afrika Kusini.Mbali ya Tanzania washiriki wengine katika shindano hilo wanatoka katika nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan ya Kusini.Lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya wasanii wa muziki nchini na hata kwa nchi za Afrika ashariki.Wawakilishi wan chi walipatikana katika usaili uliofanyika Septemba 18, kwenye hoteli ya Peacock Jijini Dar es Salaam.Septemba 25 kambi hiyo ndipo itaanza rasmi ambapo wasanii wa hapa nchini watakutana na wasanii wengine kutoka katika nchi hizo na kuanza kushindana .Majina ya wawakilishi wan chi yamepitishwa na waliokuwa majaji katika usaili ambao ni Paulo Ndunguru, Sauda Kilumanga na Hamisi Bakari.

No comments:

 
 
Blogger Templates