Social Icons

Wednesday, September 29, 2010

CCM wavamia Ofisi ya CHADEMA, Kishapu

Na Tamali Vullu, Kishapu
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, Jana walivamia ofisi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilaya hiyo na kung’oa mlingoti wa bendera na kuichana.Tukioa hilolilitokea jana katika ofisi hiyo ya chadema iliyopo eneo la Mhunze, makao makuu ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.Wanachama hao waliokuwa katika mkutano wa MgombeaUrais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, uliofanyika katika uwanja wa Shirecu, hali iliyowafanya wananachi wa kawaida waliofika katika eneo hilo kustushwa na tukio hilo.Walivamia ofisi hiyo chadema iliyopo pembezoni mwa uwanjahuo kabla ya mkutano huo haujaanza rasmi huku Kikwete, akiwa hajafika katika eneo hilo kwa ajili aya kuhutubia mkuatano huo wa kampeni.Wanachama hao waliokuwa wamevalia sare za CCM, wakiwa katika kundi kubwa huku wakiongozwa na kamanda wa, baada ya kufika katika ofisi ya Chadema, mmoja wa wanachama hao aliung’oa mlingoti wa bendera na kuutupa chini na kisha kuondoka naohuku akishangiliwa na baadae kuichana bendera hiyo.Wakati tukio hilolikitokea baadhi ya viongozi wa Chadema waliokuwapo ofisini hapowalishuhudia tukio hilo huku wakishindwa na kufanya.Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Wananawake wa Chadema Wilaya ElizabethMbuke, alielezea kusikitishwa na tukio hilona kusema wameshatoa tarifa katika kituo cha Polisi Mhunze.“Jana vijana wa CCM, walikuja na kuishisha benderana kuiweka ndani, leo wameng’oa na kuichana nimekwenda kutoa tarifa Polisi, OCD ameniambia leo ana ugeni mzito atashughulikia baadae” alisema Mbuke.Alisema kuwa juzi baada ya kushushwa bendera yao, Mkuu wa Wilaya hiyo alimpigia simu na kuomba ashushe bendera hiyo mpaka Kikwete, atakapoondoka kwani ni aibu akiikuta bendera ya Chadema ikipepea.“ Lakini DC, anapiga simu vijana wa CCM, walishakuwa wameshaishusha bendera, lakini akaniambia kama wamefanya hivyo walikosea” alisema Mwenyekiti huyo.Akizungumza katika Mkutano huo Kikwete aliwaomba radhi wakazi wa eneo hilo kwani mkutano huo ulikuwa ufanyike jana lakini akashindwa kufika kutokana na Helkopta anayotumia kupata hitilafu.

No comments:

 
 
Blogger Templates