Social Icons

Wednesday, July 28, 2010

Eric Sagala:Wachezaji wa sasa si kama wazamani

Eric Sagala mcheza soka aliyeng'ara mwanzoni mwa miaka ya 1980 na 1990 ameibuka na kudai kwamba wachezaji wa soka wa miaka hii hawana vipaji kama ilivyokuwa katika enzi zao.Sagala mabye hivi sasa ni mchezaji wa timu ya watu wazima Tanzania Stars inayoundwa na nyota wengi wa zamani ambayo huwa inacheza soka kila siku ya Jumapili katika viwanja vya Leaders Kinondoni.Sagala anasisitiza kwa kusema wachezaji wa sasa hawajitumi ipasavyo licha ya kupata sapoti mbalimbali kwa Kampuni kubwa pamoja na serikali.Katika enzi zake Eric alicheza nafasi ya winga wa kulia na alianza kucheza katika timu ya Ustawishaji Makoa Makuu Dododma CDA.Timu zingine alizocheza ni Timu ya Mkoa wa Dododma Mazengo Worriors, Simba na nje ya nchi alicheza katika timuya Township Roller's Botswana Defences Force ( BDF) ya Botswana.Eric alivutiwa kucheza soka na kaka yake Edward Sagala aliyekuwa beki namba 2 wa timu ya CDA , pia muasisi wa ofisi hiyo iliyoasisiwa mwaka 1973 mkoani Dodoma. Hivi sasa Edward ni Daktari anayeishi nchini Marekani

No comments:

 
 
Blogger Templates