Wakati huohuo babamdogo wa marehemu Mchungaji Enock Ambroseo amesema kuwa marehemu Berliss na baba yake wameingia nchini kwa miezi mitatu wakitokea Lubumbashi nchini Congo.
"Baada ya kutoa taarifa kwenye Jumuia ya Watu wa Congo tumeaamua kuwa na msimamo mmoja kwamba hatutakwenda kuchukua kibali cha mazishi ya binti yetu hadi pale uchunguzi utakapokamilika ili marehemu apate stahiki zake kwa kukatishiwa uhai"amesema Ambroseo.
Pichani ni baba wa marehemu Mchungaji Kalanba Mukala Louis ambaye ni muumini wa Kanisa la Pentecoste makaazi wa eneo la Mkuza Mharakani Picha ya Ndege Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Kibaha ,Pwani
Raia wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) wanaoishi nchini wameweka msimamo wao wa kugoma kuzika mwili wa binti Mujinga Ngalula Berliss (17) ambaye mwili wake uliokotwa hivi karibuni maeneo ya pori la Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani akiwa amefariki kwa
kuchomwa ni kitu chenye ncha kali shingoni mwake kama jinsi ilivyoelezwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya kwenye taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari.
Akizungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwake leo tarehe 26 Oktoba ,2024 eneo la Mkuza Muharakani baba wa marehemu aliyejitambulisha kuwa ameingia nchini akitokea Lumbumbashi mahsusi kwa kutoa huduma katika Kanisa la dhehebu la Pentecoste Mchungaji Kalanba Mukala Louis amesema Jumatatu iliyopita marehemu alimuaga mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 kuwa anakwenda saluni kusuka nywele na baada ya hapo hakurudi nyumbani waka kupata taarifa zozote .
"Tulimtafuta sana bika mafanikio hadi usiku nikowa n babake mdogo bila mafanikio
nilimtuma mdogo wake aende kumuulizia kwa majirani wote hawakufahamu alipokwenda nikatoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa tukashirikiana kusambaza picha zake kwa majirani na wachungaji mbalimbali siku ya Jumatano Mwenyekiti alinipigia simu na kuniambia amepata taarifa kuna mwili umeokotwa mapori ya Msangani uko Hospitali ya Rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani hivyo tukaongozana kwenda kuuangalia nilipofika chumba cha maiti nikamtambua mtoto wangu lakini nikazuiwa nisimguse kwa sababu za kiusalama niliuona mwili wa mwanangu ukiwa umerowa damu huku akiwa ametobolewa macho nimelia sana" amesema Mchungaji Louis ambaye ni baba wa marehemu Berliss.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani.Alidha aliyekua Mwenyekiti wa Umoja wa Wakongomani wanaoishi nchini Abdallah Serge amesema kwa niaba ya Umoja wao wamegoma kumzika marehemu Berliss mpaka watakapo ridhika na uchunguzi wa mauaji hayo tofauti na ilivyo sasa hawajaridhika na taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.
"Jana usiku nimempigia simu Balozi wetu wa Congo amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha binti yetu na amesema ataandika barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje kutoa malalamiko yao na kuiomba serikali ya Tanzania iweze kutoa taarifa zitakazowaridhisha ndipo ikiwemo gharama za kumstiri marehemu " amesema Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wakongomani wanaoishi nchini.
Akizungumza kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya amesema uchunguzi wa kuwabaini wahusika bado unaendelea
0 Comments