Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuingiza umeme wa upepe kwenye grid ya taifa mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau mbalimbali wa umeme.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya
kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki imesema iko kwenye mchakato wa
kuingiza umeme huo kwenye gridi ya taifa, baada ya kukidhi vigezo vya kitaifa.
Akizungumza leo Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte alisema mradi
huo unafanywa kwa ushirikiano na taasisi ya fedha ya Kimataifa iliyochini ya
benki ya dunia.
Alisema
taasisi hiyo imetoa dola za kimarekani milioni 300 kwa ajili ya kufanikisha
mradi huo mkubwa, utakaonufaisha sio tu watanzania bali nchi nyingine.
“Tutakuwa na
miradi mikubwa lakini sasa tunaelekea kuingiza upepo wa umeme kwenye gridi ya
taifa, ili tuanze kusambaza nchi nzima, watu watanufaika kwa njia ya upepo,”alisema.
Kampuni hiyo
inatarajiwa kuwa na Kongamano la nishati mbadala litakalofahamika kama ‘Off the
Grid’ kwa ajili ya kuzungumzia namna ya kuendeleza miradi mikubwa kwa kutumia
nishati mbadala.
Alisema dhamira
yao ni kuhakikisha wanakuwa na miradi mikubwa itakayofanya kazi katika nchi
zilizokusini mwa jangwa la Sahara.
0 Comments