Meneja masoko wa Kituo cha televisheni cha EATV, Roy Mbowe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza makundi mapya matatu pamoja na yaliyopita yatakayoshindaniwa katika tuzo za Eatv (EatvAwards) zinazotaraji kufanyika Desemba 10 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Godfrey Mngereza amesema
kuwa tuzo hizo zimefata vigezo vyote kwa kuwa wasanii wote ambao
wameshiriki katika tuzo hizo wamesajiliwa na basata hivyo wale wote
waliojipendekeza lakini awakusajiliwa walikuwa wanajiondoa wenyewe
kwenye mashindano kwa kukosa sifa.
Mwakilishi
kutoka Vodacom ambao ni wadhamini wa Tuzo hizo akitaja moja ya Makundi
ambao watashiriki katika kinyang'anyiro hicho, na kueleza kuwa Vodacom
itaendelea kusapoti sanaa
Wanahabari wakiwa katika Mkutano huo
Mwakilishi wa Coca Cola akishukuru EATV kwa ushirikishwaji wao katika swala zima la Sanaa na kuahidi kuwa wataendelea kusapoti
Mwakilishi kutoka Benki ya Barclays ambao ni wadhamini akielezea namna Benki hiyo itakavyo endelea kutoa sapoti katika kutoa tuzo.
Mwakilishi wa African Songs wauzaji wa muziki mtandaoni akielezea jinsi watakavyo wakuza wasanii zaidi kupitia tuzo hizo
Mwakilishi kutoka Innovex akieleza namna watakavyo simamia mchakato wote kuhakikisha haki inatendeka kwa kuhakiki matokeo
Mwakilishi kutoka Selcom akieleza kwa kina namna watakavyo simamia zoezi la upigaji kura ambalo litaanza rasmi jana usiku
Mmoja wa wanahabari akiuliza swali wakati wa mkutano huo
Wanahabari wakiendelea kupata tukio hilo
Picha zote na Fredy Njeje
0 Comments