DSTV YAMTANGAZA JOTI KUWA BALOZI WA DSTV BOMBA, WAPUNGUZA BEI YA KIFURUSHI


Balozi wa DSTV Bomba,Lucas mhavile "Joti" wa pili kulia akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Multichoice Tanzania kutoka kushoto ni Afisa Masoko Alpha Mria, Meneja uendeshaji Baraka Shelukindo na Kulia ni Meneja mauzo Salum Salum.
Meneja Muendeshaji wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Baraka Shelukindo akiongea na Waandishi wa habari wakati akimtangaza Balozi wa DSTV Bomba leo jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Vichekesho Nchini ,Lucas Mhavile “Joti” ,akitoa Shukrani zake mara baada ya kutangazwa kuwa Balozi wa DSTV Bomba leo jijini Dar es Salaam. Picha Zainab Nyamka.

KAMPUNI ya Multichoice Nchini imemteua msanii wa vichekesho Lucas Mhavile 'Joti' kama balozi wa kifurushi cha DSTV Bomba kwa kukitangaza kifurushi hicho pamoja na kutilia mkazo huduma bora zinazotolewa na kampuni hiyo katika kuburudisha na kuhudumia kwa weledi wateja wake.
 
Akizungumza wakati wa kumtambulisha balozi huyo mpya wa kifurushi cha DSTV Bomba, Meneja muendeshaji wa Multichoice Baraka Shelukindo amesema kuwa hatua hii inakuja zaidi hasa baada ya kutaka kila mteja wao afurahie huduma za DSTV kwa kushuhudia mechi za La Liga, Maisha Magic Bongo na baadhi ya mechi za EPL pamoja na kushuhudia michuano ya kombe la Mataifa Afrika kupitia Super Sport Selekt.

Shelukindo amesema kuwa, katika kifurushi cha DSTV Bomba wateja wao wataweza kushuhudia ongezeko la chaneli mpaka kufikia 77 tofauti na awali pia kutokana na maombi ya wateja wao kampuni ya DSTV wameamua kuongeza kwa chaneli ya dini ya kiislamu ya Imani TV itakayoanza kuonekana kuanzia Novemba 17.

Kutangazwa kwa balozi huyo, kunaenda sambamba kabisa na punguzo la bei kwa kifurushi hicho kutoka 23,500 mpaka 19,975 kwa mwezi na hii inakuja ili kutoa fursa kwa wateja na watumiaji wa DSTV kuweza kuendana na hali ya maisha ilivyo kwa sasa.

Meneja Mauzo , Salum Salum hii ni fursa kubwa sana kwa wateja wapya na wa zamani wa DSTV kwani watapata fursa ya kushuhudia chaneli mbalimbali za burudani, tamthilia, michezo ikiwemo michezo ya kimataifa ya Riadha kupitia SuperSport 4.

Msanii Joti amesema kuwa ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwa balozi wa DSTV Bomba kwa kipindi cha miezi sita na wameona jitihada zake katika sanaa ndiyo maana wakaona umuhimu wake katika kutangaza kifurushi cha DSTV Bomba kama balozi wao.

Post a Comment

0 Comments