Social Icons

Tuesday, July 19, 2016

TWIGA CEMENT YAZINDUA PROMOSHENI YA "JIJENGE NA TWIGA CEMENT" KWA WATEJA WAKE

Mkurugenziwa Masoko Simon Delens   akionesha mfuko wa Twiga Cement Extra ambao  uko kwenye prosheni  ya Jijenge na Twiga Cement itakayowahusisha wateja wao.

Kiwanda  cha Twiga Cement kilichopo eneo la Wazo Hill Jijini Dar es Salaam kinachofahamika kwa jina la Tanzania Portland Cement Company Ltd (TPCC) jana wamezindua promosheni itakayofahamika kwa jina la ‘Jijenge Na Twiga Cement’ itakayodumu kwa majuma nne.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kiwandani leo Mkurugenziwa Masoko Simon Delens alisema promosheni hiyo inafanyika kwa kwa mara ya kwanza na Kampuni hiyo pia haijawahi kufanywa na Kampuni nyingine yoyote ya ya uzalishaji wa cement nchini.

“Twiga Cement inajivunia kuzindua promosheni hii ya kipekee ambayo inawahusu wateja wote wa TPCC kwa kupitia promosheni hii ya ‘Jijenge na Twiga Cement’ washindi watapata nafasi ya kushinda mifuko 600 ya cement, Kampuni imetenga jumla ya mifuko 4,800 ya cement kwa ajili ya promosheni hii” alisema Delens.

Delens aliongeza kwa kusema kuwa Kampuni yao imeamua kuwazawadia wateja wake waaminifu hivyo ametoa wito waichangamkie fursa hiyo muhimu huku akizitaja zawadi zingine zitakazokuwa zikitolewa kwenye promosheni hiyo kuwa ni mashine za kufyatulia matofali, mixers, matoroli, fulana na kofia.

Delens aliongeza kwa kusema kuwa Kampuni ya Twiga Cement ndiyo inayoongoza kwenye soko la cement nchini alimalizia kwa kuwakumbusha na kuwahamasisha wateja wa Twiga Cement waendelee kununua cement wanayoitengeneza kwani endapo mteja akipata zawadi ya mifuko itamsaidia kujenga nyumba.

“Huu ni mwanzo wa safari nzuri kwani tumejipanga kwa ajili ya programu nyingine nyingi zinzkuja mwaka huu alisema”.

Akifafanua namna ya kushiri Delens alisema mara baada ya mteja kununua mfuko wake wa Twiga Extra anaona namna maalumu ya siri itakayokuwa imewekwa kwenye valvu ya kila mfuko wa Twiga na kutakiwa kuituma namba hiyo ya siri kwenda namba 0789 000 666 ambapo atakuwa ameingia moja kwa moja kwenye droo ya wiki washindi watakuwa wakipatikana kila Ijumaa.

Promosheni hii itafanyika ndani ya majuma manne itafikia kilele Ahosti 28 mwaka huu.

No comments:

 
 
Blogger Templates