Social Icons

Thursday, February 4, 2016

MAYUNGA AUBANIA WIMBO ALIOREKODI NA AKON

Msanii nyota  wa shindano la Airtel Trace Music Star , Malimi  Mayunga  amesema  wimbo wake aliourekodi  na mwanamuziki  nyota duniani  Akon raia wa Senegal, utabaki  kuwa siri hadi siku utakapotoka rasmi.

Mayunga  alisema  kwamba wimbo huo ambao umerekodiwa  nchini Marekani ni mzuri  na anaamini  utamuweka  katika  ramani  nyingine  duniani  pale  utakapotoka.

"Naishukuru Airtel  kwa  kuweza  kunitoa  katika  hatua  moja na kunipandisha  daraja  hadi kuweza kufika nchini Marekani na kunikutanisha  na mwanamuziki Akon ambaye katika mazungumzo naye akiniambia  kwamba ipo siku sauti yangu  itabadilisha maisha yangu kauli ambayo kila wakati naisikia kichwani mwangu hivyo naongea na nafsi yangu kujituma zaidi ili siku moja niwena maisha mazuri" alisema Mayunga.

Mayunga alisema Akon alimwambia kwamba ana sauti ya kipekee huku akimuuliza kama amewahi kuwaza kuishi  Marekani na kusisitiza kuwa kama atafanikiwa kutoa wimbo mmoja tu  na kulikamata soko unaweza kumbadilishia historia ya maisha yake.

Akieleza siri ya ushindi wake kwenye shibdano hilo la kuonesha kipaji cha kuimba alisema,nidhamu na kufuata maelekezo aliyokua akipewa na  walimu alipokuwa katika mashindano ndiyo siri kubwa.

Katika anga ya muziki  wa kizazi kipya Mayunga anatingisha na wimbo wake unaokwenda kwa jina la 'Nice Couple'.

Mayunga alisema hayo  katika Jukwaa la Sanaa alipokuwa akizungumza  na wadau  wa burudani  uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Jijini Dar es Salaam.

No comments:

 
 
Blogger Templates