Social Icons

Wednesday, September 24, 2014

MZEE KASSIM MAPILI ALAZWA MUHIMBILI , RAIS WA SHIRIKISHO LA MUZIKI ADDO NOVEMBER AMTEMBELEA

Kutoka kushoto ni Gwiji wa muziki wa dansi nchini Mzee Kassim Mapili akiwa amekaa kwenye kitanda cha hospitali ya Taifa Muhimbili  kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Dansi Tanzania Addo November alipokwenda kumjulia hali  leo asubuhi hospitalini hapo.

NA BONGOWEEKEND BLOGSPOT.COM

HALI ya mwanamuziki nguli Kassim Mapili aliyelazwa katika Hospitali  ya Taifa  Muhimbili katika kitengo cha moyo inaendelea vizuri imehafamika.

Mapili ambaye awali alilazwa katika Hopitali ya  Mwananyamala  kutokana na kusumbuliwa na  maradhi ya mapafu kujaa maji  pamoja na moyo kujaa maji ambako alilazwa kwa muda wa siku nne kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili juzi  mchana.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa Shirikisho la Muziki  Addo November  ambaye aliefika hospitalini hapo mapema asubuhi kumjulia hali Mapili  ambapo alikiri kuwa amelazwa katika wodi  namba moja  katika Taasisi ya Moyo baada ya kutolewa  katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU), Muhimbili.

Aidha November ametoa rai kwa wadau na wanamuziki  viongozi  mbalimbali  kujitokeza kwa wingi kwenda kumjulia hali gwiji huyo wa muziki ikiwa ni sehemu ya kumpa faraja kwa ujumla.
 “Mzee wetu anaumwa sana na amevimba sana  miguu hivyo  ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa msaada wa hali na mali” alisema November.
Wakati Mapili akiwa amelazwa mama yake mzazi  aliyetajwa kwa jina la  Hajena Mussa  Mchikita amefariki usiku wa juzi nyumbani kwake Nachingwea  na atazikwa  leo mkoani Songea alisema November .
Mapili  alitamba na nyimbo za ‘Rangi ya Chungwa’, ‘Mayasa’ ambao aliuimba na Marehemu TX Moshi William enzi za uhai wake  na kutamba vilivyo katika miaka ya 1980.

No comments:

 
 
Blogger Templates