Social Icons

Tuesday, September 11, 2012

WAANDISHI WA HABARI WANDAMANA KUOMBOLEZA KIFO CHA DAUD MWANGOSI JIJINI DAR ES SALAAM

Waandishi wa Habari  kushoto ni Mwani Nyangasa  (Mtanzania) na Esther Mbussi (Jamhuri) wakiwa  katika maandamano hayo.

 Waandishi wa Habari  kutoka kushoto Happy Mnale, Khadija Kalili  na Salum Mkandemba wote waandishi wa Gazeti la Tanzania Daima wakiwa katika maandandamano ya waaandishi wa Habari wa Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten Dau Mwangosi aliyeuawa  kwa kuripuliwa na bomu na askari wakati akiwa kazini, Katika Kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa mapema mwezi huu. 
 Mwanahabari mkongwe Leila Sheikh akiwa na wanahabari nje ya jengo la ofisi za Channel Ten , kushoto ni Mwenyekiti wa Dar es Salaam Press Club Jane Mihanji (Da Jane) na Somoe Ng'itu mwandishi Mwandamizi gazeti la Nipashe na Dkt. Azavery Rwaitama.
 Picha  ya Marehemu Daud Mwangosi. 

 Maandamano yakiendelea katikati ya jiji.






 Hapa wanahabri wakiigiza tu jinsi Marehemu Mwangosi alivyoshambuliwa na kulipuliwa na bomu


 Polisi wakitoa ulinzi kwa waandishi wa habari waliokuwa wakiandamana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi alipata wakati mgumu ambapo wanahabari walimwambia hawamuhitaji katika mkutano ule ambapo wanahabri walianadamana na kumkuta katika viwanja vya Jangwani, hata hivyo aliomba apewe maazimio laikini waaandishi pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali Vya Habari walikataa  na kumweleza kwamba wana mheshimu sana na wamekuwa wakifanya nae kazi kwa muda mrefu hivyo  alielewaq akaondoka na mambo yakaendelea na kumalizika salama salmini. 
 Igizo la shambulio likifanyika.

No comments:

 
 
Blogger Templates