Social Icons

Wednesday, August 29, 2012

WASANII WATAKIWA KUJIENDELEZAKITAALUMA

Mkufunzi wa masuala ya aundaaji wa Filamu kutoka taasisis ya Sanaa na uandishi wa Habari (IAMCO) Ngalimecha Ngahyoma, akizungumza jambo katika Jukwaa la Sanaa, kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego

Na Mwandishi Wetu
Wasanii wanchini wametakiwa kujiimarisha katika masuala ya taaaluma ili waweze kufanya kazizenye ubora na zinazokidhi mahitaji  yasoko la ndani na nje ya nchini.

Akizungumzakatika Jukwaa la Sanaa jana, mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa filamu hapanchini Ngalimecha Ngahyoma amesema kumekuwa na matatizo mengi katika uandaajiwa kazi za filamu hapa nchini kutokana na wasanii kutokuelewa misingi yauandaaji wa filamu.

 “Kuna maeneoya msingi ambayo yanahitaji watu kubobea ili kuyafanya kwa utimilifu, na hakunanjia ya mkato ni lazima kuyapata shuleni kwa maana lazima mtu ufundishwe.Wasanii wengi wanatumia vipaji vyao, lakini matokeo ya kufanya mambo kwa vipajindiyo haya ambayo yanatupa filamu zenye matatizo katika maeneo mbalimbali,”alisema.

Alisema nimuhimu kwa wasanii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuanza kuandaakazi kitaalamu ili kufanya kazi zilizobora na kwamba ni vyema kutumia wataalamkatika maeneo yote yanayohitaji utalaam badala ya mtu mmoja kufanya kazi zote.

 Kwa upandewake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego,amesema suala la taaluma alikwepeki katika kutengeneza kazi zenye ubora nakuwasisitiza wasanii kujiunga na vyuo kupata utaalam katika fani zao.

No comments:

 
 
Blogger Templates