Social Icons

Wednesday, July 25, 2012

CHAMELEON KUTOKA NA SEAN KINGSTONE


NYOTA wa muziki kutoka nchini Uganda na Afrika Mashariki , Joseph Mayanja 'Chameleon', amesema yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya ambao bado hajaupatia jina na amemshirikisha msanii kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Jamaica, Sean Kingstone.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chameleon alisema anavutiwa sana na kazi za Sean Kingstone ndio maana ameamua kushirikiana nae katika wimbo huo ambao anaamini utakuwa gumzo kwa kila nchi.

“Sean Kingstone ni msanii ambaye namkubali sana, kazi zake nyingi huwa zinafanya vizuri, hivyo nimelazimika kumlipa kiasi cha fedha anazohitaji ili kufanikisha malengo yangu, nimemlipa milioni 45 za Tanzania, kwa kazi aliyonifanyia hivyo namshukuru sana” alisema Chameleon.

Alisema, anawaomba mashabiki wa kazi zake wakae mkao wa kula kwa kuupokea wimbo huo, kwani anaamini utafanya vizuri kutokana na kuwepo kwa msanii huyo wa kimarekani.

No comments:

 
 
Blogger Templates