Social Icons

Wednesday, June 27, 2012

WAREMBO WABUNGE DOM KUPALILIA SHAMBA LA TWANGA IJUMAA KILIMANI CLUB

Wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta  Asha Said 'Sharapova'na Mary Kimwana wakikamua.

BENDI ya The African Stars 'Twanga Pepeta' Ijumaa ya wiki hii tarehe 29-06-2012 itatoa burudani katika kinyang'anyiro cha kumsaka Redd’s Miss Kanda ya Kati onesho litakalofanyika Mkoani Dodoma.  
Onyesho hilo limepangwa kufanyika  katika ukumbi wa Kiliman Klab maeneo ya Uzubguni   ambapo litawakutanisha warembo waliopatikana katika mikoa ya Kanda ya Kati kutoka katika Mikoa ya Redds Miss Tabora, Redds Miss Singida, Redds Miss Dodoma na Redds Miss Kigoma ambayo yalifantika katika hatua za awali na kuwapata wawakilishi watatu kila mkoa. 
Akizungumza na Bongoweekend Mratibu  bendi ya Twanga Pepeta Hamisi Kayumbu ‘Amigolas’ alisema bendi hiyo itatumia fursa hiyo  kuitambulisha single yao iliyokamata Jiji kwa sasa ya 'Shamba la Twanga' kwa wapenzi wake wa Dodoma pia tunataraji kuwaalika Waheshimiwa Wabunge wanaohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea mkoani humo . 
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shindano hilo. 
Twanga Pepeta wataondoka Ijumaa alfajiri mara baada ya kumalizika kwa tariba ya onesho lao la Club Maisha linalorindima kila siku ya Alhamisi  na watarejea jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi ambapo watatoa burudani katika ukumbi wao nyumbani wa Mango Garden au maarufu kama 'Twanga City'. 
“Bendi hiyo itapeleka kundi lake lote ambapo tunataka kufikisha sal;amu kwamba sisi ni kisima cha burudani au kwa lugha nyingine unaweza kusema kwamba ‘Twanga sawa na Kisima cha kale’ hakikauki maji  hivyo wakazi wa mkoa wa Dodoma na wadau wengine pamoja na Wabunge watapata burudani nzuri kutoka kwa wanamuziki waliosheheni vipaji na wanamuziki nyota watakaoongozwa na Meneja wa Bendi Khamis Amigo na Kiongozi Luizer Mbutu.

No comments:

 
 
Blogger Templates