Social Icons

Tuesday, January 31, 2012

ISHA MASHAUZI AJA KIVINGINE,ANASEMA KAMA YEYE AMEPINDA WENZAKE TUMEJISOKOTA

Al anisa Isha Mashauzi  ambaye ni Mkurugenzi wa Mashauzi Classic katika picha.

Siyo  Isha yule aliyezoeleka kwa nyimbo za kumshtakia Mungu, mapenzi na zile za kumtukuza mama, Isha wa leo ameshuka na mipasho mikali itakayokuwa mwiba kwa yeyote atakayelengwa na mashairi yake.

Isha anakuambia tumpepee mleteni mbele tumzodoe tusimwache tumkomeshe, kama yeye chizi wenzake tumewehuka, tunanyamaza kwa shari zake kuziepuka, kama yeye amepinda wenzake tumejisokota, kama ni kujichetua darasa liko mtaani kwetu tunazijua kero shari na ugomvi kuutafuta.

Ni wimbo mkali ambao utazidi kumuweka Isha kileleni  ambaye ni miongoni mwa waimbaji wenye mvuto na mahiri  wa taarab hapa nchini.

Huu unakuwa ni wimbo wa kwanza kwa Isha ndani ya kundi la Mashauzi Classic tangu lianzishwe miezi michache iliyopita mwwaka jana

Ukiuskiliza wimbo huu utakutana na  misemo mingi ya kuvutia kama vile Ng’ombe aliyewahi hanywi maji yaliyochafuka, Usichane mtihani kabla mwalimu hajasahihisha, Kama unapenda samaki basi usichukie wavuvi.

Aidha katika wimbo huu Isha ameonesha ukomavu mkubwa katika uimbaji ambapo mbali na kuimba kwa hisia kali pia ameweza kucheza sana na sauti yake, kuna wakati  ame rap huku akinguruma mithili ya simba hali iliyopelekea mtangazaji mmoja wa kituo cha redio kusema “Hii inaitwa iga ufe”

No comments:

 
 
Blogger Templates