Social Icons

Thursday, September 8, 2011

ZIJUE SABABU ZA KUACHWA, OKEREKE , MONALISA CHINDA NA STELLA

ASALAM alleykum wapenzi wa safu hii ya nyota wa Nollywood ambayo hukupatia nafasi ya kujua matukio na historia za waigizaji wa Nollywood.Katika makala hii tutakwenda kuangazia sababu kubwa ambazo zimekuwa zikiwakumba wasanii wengi wa nchini hapa kuachika mara baada ya kuolewa.

Katika makala hii tutakuwa na wasanii Stella Damasus, Stephanie Okereke, Monalisa Chinda, Eucharia Anunobi na wengine.

Katika makala hii kwa kutumia mifano ya waigizaji hao mwandishi alifuatilia hasa sababu za watu hawa maarufu kuachwa mara baada ya kuolewa.
 Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao wa www.nigeria.com umeonyesha sababu ya wengi kukumbwa na dhahama hiyo.
 Mwanzo wa mapenzi yao yanakuwa ya furaha lakini baada ya hapo wanajikuta wakiishia katika maumivu makali ya kuumizwa
.Wataalamu hao wameeleza kuwa mamilioni ya wanaume wamekuwa wakiwatamani waigizaji badala ya kuwapenda.Akitoa mfano kwa mfano mwigizaji, Stella Damasus, alijikuta katika tatizo hilo baada ya kufariki kwa mumewe, Jaiye Aboderin, amejikuta katika wakati mgumu kwenye mahuasiano kutokana na kupata wanaume na baada ya muda mfupi anajikuta akiachwa na kubaki kuumia moyoni na hivi juzi amejikuta akiishi kulizwa na Prince aliyekuwa ametangaza kufunga naye pingu za maisha mwakani.Mwigizaji mwingine aliyejikuta katika ombwe hilo ni Stephanie Okereke, aliyeumizwa na aliyekuwa mpenzi wake mcheza soka, Chikelue Iloenusi

.Mcheza soka huyo alimuacha na kumrejea mpenzi wake wa zamani mara baada ya kumpatia penzi lake.Kwa upande wa Monalisa Chinda alitengana na mumewe kutokana na kutokuwa mwaminifu ikiwa ni pamoja na kumpiga, kumdhalilisha mbele ya jamii bila kujali umaarufu wake.Upande wa Eucharia Anunobi kesi yake haina tofauti na za hawa waliopita kwani mumewe alimtelekeza huku akimuacha na mtoto mlemavu na kwenda kumrejea mchumba wake wa zamani wa nchini Mjerumani.

 Watafiti wa masuala ya ndoa na mahusiano wamesema kuwa wengi wa wanaume wanaowaoa wamekuwa wakiwatamani hawa kutokana na umaarufu wao na wengi hawana mapenzi ya kweli kwa wasanii hawa. Hali hii imechangia kwa kiasi kikubwa wanaume hawa pindi wanapowapata wasanii katika mahusiano au ndoa kuwaacha na kuhamia kwa wanawake wengine wanaowapenda.

 Wengi wa wanaume hao wamekuwa wakifurahia kuonekana nao kwa kujionyesha kwa watu wengine wanaokuwa wanawaona nao.Tatizo linalokuja kwa wasanii wengi hujikuta wakiwapenda kwa moyo wote wanaume hawa wanaojitokeza ambao hutumia udhaifu huo kuwatesa.

Wasanii wengi wamekuwa wakiingia kichwa kichwa katika masuala la mahusiano bila ya kufanya uchunguzi wa historia za nyuma za wanaume hao kabla ya kuwapatia nafasi ya kuwapenda.

Tatizo hilo si kwamba limekuwa likiwakuta wasanii kutoka Nigeria yenyewe bali huwa linawakuta wengi duniani.

Ukiachilia hawa wa Nigeria wengine wa nje ambao wamekuwa wamekumbwa na tatizo hilo ni pamoja na Halle Berry aliyempatia moyo wake Dwayne Wade ambaye baadaye akaanza kuonyesha vitimbwi. Wengi wa wasanii wamekuwa wakitamani kuishi bila dosari katika mahusiano yao lakini tatizo limekuwa ni kukurupuka kukubali kuolewa na watu wasio wajua kisa ni matajiri au wamewatamkia wanawapenda.
 Monalisa Chinda.
 Okereke.
Stella Damasus.

No comments:

 
 
Blogger Templates