Social Icons

Monday, September 19, 2011

MAHAFALI YA SITA NYUMBA YA KUKUZA VIPAJI YAFANYIKA DAR ES SALAAM

 Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya muziki  mwaka 2011,katika nyumba ya vipaji Tanzania House Of Talent THT , wakisubiri kulishwa keki inayokatwa na mwanamuziki mkongwe  pia mmoja wa waalimu wa THT Kadinali Gento.Hafla hiyo ilifanyika THT-Kinondoni Block 41 Jumapili.
 Kadinali Gento akikata huku akishuhudiwa  na badhi ya wahitimu.
 Mwalimu Nkya akimlisha keki mhitimu wa THT, huku tukio hilo likishuhudiwa na Gento.
 Baadhi ya wahitimu wakisikiliza neno.
 Gento akiwa tayari kumlisha keki mhitimu.
 Ticha Nkya akilishwa keki,kulia ni Gento.
 Mahafali  hayo yalihudhuriwa na na watu mbalimali akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars Entertainment inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta Sugu Asha Baraka, 'Iron Lady', anayefuata ni Mwalimu wa THT, Nkya na Khadija aliyekaa.
 Mwanamuziki wa siku nyingi Kalora Kinasha akiselebuka na Mwasiti Almasi ambaye ni zao la THT.
 Mlezi wa wana Asha akiwa na mtoto Fetty.
 Fetty kushoto akiwa na Mamie Khadija.
 Mwasiti  akiwatambulisha wasanii wapya wa THT jukwaani ambapo wageni waalikwa walifurahia kuona vipaji vyao siyo vya kubabaisha kwani kila mmoja alikuwa na umahiri wake.
 Msanii mchanga kutoka kitaa cha Temeke  Aslai akionyesha ujuzi wake katika mahafali hiyo pembeni yake ni Ditto. 
 Msanii mpya Khalid akiimba wimbo wake wa 'Kina mama Sasambu' katika mahafali hayo ambapo na yeye ni mmoja kati ya wahitimu zaidi ya 20 wa mwaka huu.
Hapa tukiwa miongoni mwa waalikwa ambapo wimbo wa sasambu wa Khalid ulikonga na kunyanyua watu katika viti na kulazimika kucheza mduara.

No comments:

 
 
Blogger Templates