Social Icons

Tuesday, March 15, 2011

JESHI LA POLISI WAZUIA MAANDAMANO YA AMANI

Juu ni moja kati ya Vipeperushi vilivyosambazwa Jijini ikiwa ni katika sehemu ya kuhamasisha watu waweze kujitokeza katika maandamano hayo ambayo yamesitishwa na Jeshi la Polisi leo alasiri.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesitisha maandamano yaliyoombwa na Kamati ya Vijana ya Watanzania wapenda Amani yaliyokuwa yafanyike kuanzia Mnazi Mmoja hadi Balhresa Manzese , isipokuwa limeruhusu kufanyika kwa mkutano wa hadhara tarehe 16/03/2011 katika viwanja vya Bakhresa Manzese.

Hiyo ni kwa mujibu wa Jeshi la Polisi kubaini kuwa maandamano hayo yana muitikio wa watu wengi na yanaweza kusababisha msongamano ambao ungetokana na kufungwa kwa barabara kwa muda mrefu na kusababisha kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Hivyo Jeshi la Polisi tumeridhia kufanyika kwa mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Bakhresa Manzese, pia tunaahidi kutoa ulinzi wa kutosha ili mkutano ufanyike kwa amani na utulivu.

F.C Ngonyani-ACP
KNY: KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM YA POLISI
DARES SALAAM

No comments:

 
 
Blogger Templates