Social Icons

Tuesday, February 1, 2011

WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA FREE MEDIA NA BILICANAS GROUP WAKARIBISHA MWAKA KWA SHANGWE



Mhariri Mkuu Mtendaji wa Magazeti ya Tanzania Daima na Sayari Absalom Kibanda wakwanza kushoto, Mwenyekiti wa Makampuni ya Free Media na Bilicanas Group Freeman Mbowe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hizo Dk. Lilian Mtei Mbowe hawpa wakiiinua glass zao juu kuashiria ufunguzi wa sherehe ya kuuona salama 2011 katika hafla iliyofanyika Jumatatu usiku kwenye ukumbi wa Cassa Complex Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Mbowe aiongezea mtaji Free media Saccos
***********************************

Mbowe aiongezea mtaji Free media Saccos
Mwenyekiti wa makampuni ya Bilicanas Co.Group na Freemedia Ltd, Freeman Mbowe, ameahidi kutoa mtaji wa kutosha kwa kila mfanyakazi kwa ajili ya uanzishwaji wa “Freemedia Saccos” inayolenga kutoa fursa zaidi za mikopo kwa wafanyakazi wa kampuni hizo.
Mbowe aliyasema hayo usiku wa kuamkia jana wakati wa sherehe maalum ya kuukaribisha mwaka 2011 na kupongezana ambazo ziliandaliwa kwa pamoja na viongozi wa kampuni hizo wakiwemo wale wa Freemedia Ltd inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari.
Katika shughuli hiyo, Mbowe aliwaomba wafanyakazi kuendelea kujituma pamoja na kukabiliana na ushindani wa kibiashara sambamba na kuhakikisha wanafanikiwa kuendesha maisha yao kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya kujipatia kipato.
“Kilio chenu nimekisikia, ni hakika wakuu wenu wa idara wanakamilisha taratibu zote ili kuondoa matatizo yaliyopo, na jambo la msingi ni uwepo wa SACCOS, nimelipokea na nawaahidi nitawasaidia kwa hali na mali,” alisema Mbowe.
Alisisitiza kuwa atatoa wataalam wa kushughulikia suala hilo na mtaji wa kutosha kwa SACCOS hiyo.
Katika shughuli hiyo wafanyakazi kutoka idara zote za makampuni hayo matatu walikutana kwa pamoja na familia zao na kuweza kubadilishana mawazo pamoja na kusherehekea.
Mwandishi Mwandamizi wa Tanzania Daima Happiness Katabazi akigongesha glass na Mhariri Mkuu Mtendaji wa Tanzania Daima Absalom Kibanda.
Irene akimimina Shampeni kwa Mwenyekiti.
Mkurugenzi akicheza na baadhi ya wafanyakazi wake hapa ilikuwa ni katika miondoko ya kwaito. Mkurugenzi wetu Dk. Lilian Mbowe akifurahi na wafanyakazi wake.
Jinsi ninavyopenda nakshi nakshi Happy alinipagawisha na Swagga hili la mkonono.
Nuru, Dija, Dina na Irene.
Anaitwa Nuru Yanga 'Mwana Tanga' mwandishi wa habari za Mahakamani na kijamii zaidi.
Hellen Pendo Ngoromera .
Dija na Irene Maua ya Freemedia.
Meza Kuu.
Mhariri wa Michezo na Burudani Tullo Chambo a.k.a Mzee wa Kula Dawa akiwa katika tukio muhimu la kupata msosi.
Muddy Boy 'Mnyanmwezi wa Ukweli' ambaye anapatikana katika Idara ya Ulinzi Club Bilicanas na Freemedia.
Bosssssssssssssssss.
Shaban Matutu hapa akisevia supu kabla ya kupata msosi wa nguvu.

Mmoja wa wahariri makini wa Tanzania Daima Edward Kinabo kushoto na Adam Mwenge wakipata mlo.
Nikigonganisha glass na Mkurugenzi wetu Dk. Lilian Mbowe .
Nikaenda meza kuu.
Mimi na Matutu huyu ni mtu ambaye tumekuwa tukifanya kazi katika Idara ya Habari za Burudani kwa zaidi ya miaka mitatu najivunia katika hilo, ukitaka kuona mambo yake yeye nu mfasiri wa habari za burudani za nje katika gazeti la Tanzania Daima kila siku, mwana safu Tanzania Daima kupitia jarida la Wikiendi linalotoka kila siku ya Ijumaa, mchambuzi wa filamu hasa za Bongo kadhalika ana safu katika gazeti linalotoka mara mbili yaani Alhamisi na Jumapili la Sayari.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari Freeman Mbowe akitost kinywaji na wafanyakazi wake ambao pia wote ni wanahabari usiku wa kuamkia leo katika sherehe ya kufana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Cassa Complex ,Mikocheni Kwa Nyerere Jijini Dar es Salaa.Hafla hiyo pia ilikuwa na sura mbili ambapo pia alipongezwa kwa ushindi wake wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Hai Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mheshimiwa Mbowe akitoa hotuba kwa wafanyakazi wa Free Media na Bilicanas Group pamoja na wageni waalikwa.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Tanzania Daima na Sayari Absalom Kibanda katikati akimkabidhi zawadi ya Kifimbo Mh. Mbowe katika hafla hiyo anayeshuhudia ni mkuu wa ulinzi Club Bilicanas almaarufu kwa jina la Power.

Kuselebuka ilikuwa kama kawa kama dawa lakini hapa nilitoa kampani kwa muda mfupi tu mimi nilikwenda mtunza noti kwani jamaa ananyonga wee acha tu jamaa huyu ni baunsa wa Club Bilicanas.

Mwili haunawiri hivi hivi ni kwa misosi.
Mheshimiwa Mbowe akiwa na Charles Mbowe.

Mwenyekiti wa Makampuni ya Bilicanas Group , Freeman Mbowe (Wa pili Kushoto),akijumuika na wafanyakazi wa Kampuni ya Freemedia, inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, wakati wa sherehe za kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha 2011 kwa wafanyakazi wa makampuni hayo na pia kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa Hai iliyofanyika usikuwa Jumatatu.
Shampeni zilifunguliwa.
Wafanyakazi wa Club Bilicanasa hawakubaki nyuma hapa Terminator na dada walikamua haswaa.
Ni kama anajisemea hivi nyie chezeni tu lakini mimi mziki wangu huu hapa Ilikuwa ni kula, kunywa, kucheza mpaka lukwili.

Mimi kushoto Saum Abdulkheir mwenye nguo ya pink na Irene Mark.
Mkurugenzi Dk. Lilian akikata sehemu ya ndafu .
Rose bibi fedha na Marcus Mkuu wa Idara ya Usambazaji wote wafanyakazi wa Freemedia.
Mhariri Mtendaji wa Tanzania &Sayari Absalom Kibanda kushoto akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Free Media Dk. Lilian Mtei Mbowe.

Kibanda akionyesha zawadi aliyotunukiwa Mh. Mbowe.

Kamati ya mnuso huo kutoka katika Idara zote za Bilicanas Group na Freemedia hapa wakisalimia wageni waalikwa.
Irene Mark katika moja ya pozi ukumbini humo.
Cheeeeeersssssssssssssssssss.

Mambo ya maakuli yalikuwa siyo ya kuuliza.
Hapa nikiwa na Bosi Kibanda.
Happiness Katabazi anaonyesha swaga lake la mkono acha nipagawe nalo mambo ya ya Zanzibar.
Haji Kalili ambaye yuko katika kitengo cha Kompyuta (MSANIFU KURASA) na Khadija Kalili.
Mimi na Katabazi.

waliokuwa washereheshaji katika hafla hiyo Said Maiko ambaye pia ni mchora vibonzo 'Wakudata' na Mussa Ngarango mchora vibonzo Ngarango Jr.
Wadau hawa wakiwa katika hafla hiyo.
Dina na Dija Mashistito.
Maria kushoto na Dina hapa wakiwa ndiyo wamewasili .

Da Rose kushoto na mimi.

Maria Kayala Mwanatanga.
Dina mama Pipiro akiwa nje ya ukumbi mara baada ya kuwasili.

Nimekunja mikono yangu ikiwa ni ishara ya shukrani ,Asante kwa wote waliochangia katika kunipendezesha nikianza na nywele hiyo ni Less wig kutoka Maduka ya ShearIllusions yanayopatikama Millenium Tower na Mlimani City Jijini Dar es Salaam.Zipo dizaini nyingi inategemea na jinsi mwenyewe utakavyopenda kadhalika make up ni aina ya Mabelline inapatikana katika maduka yote ya ShearIllusions haina muwasho wala haikuachii harara usoni kama zilivyo poda nyingine hii haijachakachuliwa ,Vazi likiwa limebuniwa na Zahra Saloon Kinondoni.

3 comments:

MICHUZI BLOG said...

hatualikani?? acheni uchoyo nyie...

Anonymous said...

hope sasa mbowe atakua akitembea na kifimbo dat nice, nice to see also my brother Matutu you looked good dat day!!!!!!!!!!!!

Wadau-ndanda said...

Hongereni wadau kwa kuendelea kupigana katika fani. Mlipendeza na ninawatakia kila la kheri katika mwaka wa 2011.

- Eric
Mhariri mwanzilishi SAYARI, Mhariri wa Michezo Tanzania Daima, Free Media Ltd 2004-2007).

 
 
Blogger Templates