Social Icons

Friday, September 24, 2010

Mustafa Hassali kushuhudia mitindo New Arusha Hoteli

Visura 10 kuonesha mavazi yaliyooneshwa na Mustafa Hassanali nchini Cameroon February na Zanzibar Julai 2010. Mwanzilishi na muandaaji wa jukwaa la wanawake wajasiriamali Tanzania (TWENDE ) na Jukwaa la kukuza vipaji vya wabunifu chipukizi Swahili Fashion Week, ambae pia ni mbunifu maarufu wa mavazi, Mustafa Hassanali amealikwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya mavazi yanayofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku mbili tarehe 23 na 24 ya mwezi huu katika hoteli ya New Arusha. Maonyesho hayo yameandaliwa na Maridadi. Maridadi ni kikundi kinachojumisha wanawake watatu kutoka mataifa tofauti ya Tanzania, Austarialia na Uholanzi ambao wanaishi nchini katika jiji la Aruha na kujishughulisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na mendeleo ya mwanamke. Akielezea lengo la kuandaa maonyesho hayo, mmoja wa wanawake hao, Lilian Bulengo amesema kuwa “dhumuni kuu la kuandaa tukio hili linalojulikana kwa jina la “Maridadi Women Show” ni kuwakutanisha pamoja wanawake kutoka maeneo tofauti ya Arusha na Moshi katika Fashion Show, maonyesho ya biashara pamoja na kupata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali yanayowakabili wanawake katika maisha ya kila siku hapaTanzania ikiwemo suala la unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji, wanawake na kuondokana na utegemezi na masuala ya uchumi na biashara kwa ujumla”.Mustafa Hassanali, pamoja na kuwa mgeni rasmi, pia ataonyesha mavazi ambayo kwa mara ya kwanza alionyesha nchini Cameroon mezi wa 2 mwaka huu katika show iliyojulikana kama PARFUM D’AMOUR, na mavazi yanayojulikana kwa jina la Karafuu collection aliyoyaonyesha julai 2010 Zanzibar. Jumla ya visura 10, kati yao nane kutoka Dar es salaam na wawili kutoka Arusha watapita jukwaani na kuonyesha mavazi hayo ya Mustafa Hassanali, ambayo yanawavutia wengi kutoka na ubunifu wa hali ya juu. “Nimefurahi sana kupata fursa ya kuwa mgeni rasmi katika tukio hili, pia kuonyesha nguo zangu ambazo zilipendwa sana Cameroon, naamini pia wakaazi wa Arusha watafurahia kazi yangu” . Alisema Hassanali. Katika maonyesho haya Mustafa ataonyesha na wabunifu wengine kutoka Arusha ambao ni Shwari Collectables,Hanifa Hash na Woolworth.

No comments:

 
 
Blogger Templates