Social Icons

Thursday, September 16, 2010

DK.BILALI NA KAMPENI YA MTU KWA MTU.

Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata, baada ya kuwasili mpakani mwa Wilaya ya Singida Vijijini akitokea Wilaya ya Manyoni leo Sept 16. Kulia ni Mbunge Mteule wa Viti maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Bi Mariam Lazaro (90) mkazi wa Kijiji cha Dung’unyi, kumuombea Kura mgombea Udiwani wa Kata mpya ya Dung’unyi, Bwana Bruno, (kushoto) wakati msafara huo ukipita katika kijiji hicho kuelekea Makiungu Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida leo Sept 16 katika mkutano wa kampeni.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Bi Mariam Lazaro (90) mkazi wa Kijiji cha Dung’unyi, kumuombea Kura mgombea Udiwani wa Kata mpya ya Dung’unyi, wakati msafara huo ukipita katika kijiji hicho kuelekea Makiungu Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida leo Sept 16 katika mkutano wa kampeni.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, akipiga gitaa la besi katika Jukwaa la bendi ya Vijana Jazz, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani katika mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, uliofanyika kwenye Uwanja wa Makiungu mjini leo Sept 16. Picha zote na Muhidin Sufiani.

No comments:

 
 
Blogger Templates