Meneja Mkuu wa Shamba
hilo Dk. Ahmed Eltigani Al Mansour alimueleza Rais Dk. Shein na ujumbe wake
jinsi ya shamba hilo linavyofuga ngombe kwa kutumia teknolojia ya kisasa
ikiwemo kuwawekea viyoyozi na mafeni maalum kutokana na mazingira ya hali ya
hewa ya ukanda huo.
Kwa mujibu wa maelezo ya
Dk. Ahmed shamba hilo lina ngombe 12,500 ambapo kwa kila ngombe mmoja kwa siku
hutoa lita 60 za maziwa na kutoa lita 250,000 kwa siku huku akitumia fursa hiyo
kueleza siri ya mafanikio hayo ikiwa ni pamoja na utafiti mkubwa walioufanya
kabla ya kuazisha ufugaji huo.
Dk. Ahmeda alieleza kuwa
ufugaji wanaoufanya ni ufugaji bora duniani na pia ni eneo lililopata mafanikio
makubwa ikifananishwa na ufugaji unaofanyika katika maeneo mbali mbali zikiwemo
nchi za Afrika na hata nchi zilizoendelea ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa
wingi.
Akimaliza ziara yake
katika eneo hilo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi wa Al Rawabi kuwa
Zanzibar itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mashirikiano yanakuwepo
katika sekta hiyo ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kupanua wigo na kujifunza jinsi
ya mafanikio hayo yalivyopatikana.
0 Comments