BALOZI WA UINGEREZA NCHINI ATEMBELEA SHULE DODOMA

 

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah Cooke akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu  Elimu Kata ya Msalato Ally Swalehe juu ya mfumo wa taarifa  shuleni, ambapo mpango umetoa tablet kwa walimu wakuu na waratibu elimu kata. Kushoto kwake ni afisa elimu Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalato wakiimba wimbo wa kumkaribisha  Balozi wa Uingereza Nchini alipotembelea shule hiyo.


    Wanakijiji wa Chihanga ambao walihamasika na programu ya kuinua ubora wa elimu Nchini na kuanzisha kituo cha utayari kwa watoto wao ambao walikuwa wanashindwa kwenda kwenye shule mama kutokana na umbali,  wakicheza ngoma ya kigogo kumkaribisha Balozi.

Balozi Sarah Cooke akiwa na watoto wa kituo cha utayari cha Chihanga ambapo kabla ya hapo watoto hao walikuwa nyumbani , uwepo wa kituo hicho umewawezesha watoto kufurahia michezo mbali mbali kama vile kuimba na kujifunza maneno ya Kiswahili ili wawe tayari kwa kuanza darasa la kwanza. Kituo kilianzishwa mwaka jana na hii ni awamu ya pili ambayo ina jumla ya watoto 64

Post a Comment

0 Comments