KABUDI AWAONYA WATANGAZAJI KUACHA KUBANANGA KISWAHILI




Na Eugenia Kimolo ,Dodoma 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amewaonya watangazaji wa vyombo vya habari kuacha kubananga lugha ya Kiswahili na kujenga utamaduni wa  matumizi sahihi ya lugha Kiswahili.

Akizungumza Jijini Dodoma leo tarehe 13 kwenye Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa Kabudi ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema baadhi ya watangazaji wamekuwa wakipotosha umma kwa kutamka matamshi yasiyo sahihi huku akitolea mfano  wa neno 'apa' badala ya hapa, 'uyu' badala ya huyu huku ni kupotosha wananchi.
"Tanzania tumefubaza Kiswahili kwa kudumaza kwa maneno kadhaa, kubananga Kiswahili matokeo yake watumiaji wengine wa nchi zingine wanaona hatuzungumzi Kiswahili kwa ufasaha, 

"Watangazaji mna jukumu la kuhakikisha mnatangaza kwa lugha fanisi na fasaha.
Vyombo vya Habari mna mchango mkubwa wa kusahihisha makosa mkiendelea hivyo, hilo ni janga litaigharimu nchi na kuacha kuwa  kinara"amesema Prof. Khadija. 
Amezitaka  mamlaka zinahusika kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawazingatii maadili ya matamshi ya Lugha fasaha ya Kiswahili.

Profesa Kabudi amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuweka vipindi vya kuelimisha kwa wingi kuliko kuweka burudani na michezo kwa muda mwingi na kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawawezi kutamka kiswahili kwa ufasaha.   

Post a Comment

0 Comments