Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba, Elizabeth Michael a.k.a Lulu (pichani) amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana/kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.
Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.
Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.Muigizaji huyo aliletwa Mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambapo huku akiwa maevalia gauni refu na kujitanda mtandio ukiomfunika huku akiambatana na maaskari wawili wa kike ambao walivaa kiraia huku ikiwa ni vigumu kwa wanahabari na hata watu waliokuwepo Mahakamani hapo kumgundua kwa urahisi.
Kadhalika ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya Suzuki Grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.
Mara baada ya Waandishi kupigwa chenga ya mwili walikwenda kuthibitisha hayo kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Mkoa wa Kinondoni ACP Charles Kenyela alisema "ni kweli Lulu amefikishwa Kortini kama walivyosikia huku akisema Jalada la Kesi hiyo mlilipelekwa kwa DPP Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sasa ninavyozungumza tayari Lulu ameshapelekwa Rumande Segerea".
0 Comments