Social Icons

Wednesday, November 15, 2017

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO


Dar es Salaam, Novemba 15.2017

Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumapili ya tarehe 19.2017.Kambi hiyo ya siku moja itatoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi na kwa mara ya kwanza itaendesha vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa kambi ya matibabu Bwana Frédéric Morel amesema amefurahishwa na maandalizi ya mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita. “Tumefurahishwa na ushirikiano tunaopata kutoka kwa makampuni na watu binafsi katika kuhakikisha kambi hii inafanyika kwa mara nyingine tena.pili, tunatarajia idadi ya watu kuwa mara mbili kulinganisha na mwaka uliopita”.Alisema, Morel. mbali na kambi ya Kerege, klabu yetu pia mwaka huu imetoa huduma ya matibabu ya bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msasani A. Hivyo tunaomba wakazi wa Kerege na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.” Frédéric Morel.

Kwa upande wake Rais wa klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam, Anne Saels, amesema kuwa kuwa kambi hii ni mfano wa huduma Za Rotary kwa jamii. “kutoa huduma za afya kwa watu takribani 2000 hufanywa pindi watu wanaojitolea kukutana pamoja na kushirikiana kufanya kazi ili kubadilisha maisha ya wengine kuwa bora. Mwisho, uhalali wetu kama Rotary hupimwa kwa na huduma tunayotoa na tunajivunia kuwa na uwezo wa kuandaa Matibabu ya Matibabu mwaka baada ya mwaka”.Alisema, Anne Saels.

Mbali na hilo, Mwakilishi kutoka benki ya Diamond Trust, Bwana Sylvester Bahati amesema ushirikiano na klub ya Rotary ya Oyster Bay katika miaka mitano iliyopita umekuwa ni ushrikiano mzuri wenye kubadili maisha ya watu.

“Mpaka sasa zaidi ya watu 1000 wamepatiwa huduma bora za kiafya katika kambi hii na kuhimiza watu kujitolewa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii zao.Jeshi la wafanyakazi wa matibabu litakalo kusanyika siku ya tarehe 19.11.2017 haliwezi kupatikana popote kama kikundi wakati wowote ule, hii inafanya kambi ya matibabu ya Kerege kuwa ya kipekee na takribani watu 25 kutoka benki ya DTB hujitolea kila mwaka katika kambi.”Alisema ,Bwana Sylvester Bahati.

Kambi hii ya matibabu itafanyika kwa udhamini wa benki ya Diamond Trust, Whitedent, kampuni ya vinywaji ya Peps, Securex , ICAP kutoka chuo cha Colombia, pamoja na madakatri na wanafunzi kutoka Chuo cha kumbukumbu cha Herbert Kairuki, chuo kishirikishi cha afya cha MUHAS, na makundi mbalimbali kutoka asasi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali.

Klabu ya Rotary ya Oysterbay imeanzishwa mwaka 2009 na kwasasa ina wanachama 62. Ni klabu kubwa kati ya klabu 7 za rotary zinazopatikana Dar es Salaam. Klabu ya Rotary imekuwa ikiisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali baadhi yake kati ya hiyo miradi ni pamoja na Kambi ya matibabu kwa shule ya Msasani , Mradi wa vijana Poa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rotary Dar Marathon, “Rotary Mission Green” mradi wa kupanda miti, na kwasasa Rotary inajiandaa kuja na mkakati mpya utakaofanya kazi ya kuiisaidia jamii moja kwa katika maeneo mbalimbali tofauti na huduma za afya.

No comments:

 
 
Blogger Templates