Social Icons

Thursday, August 3, 2017

STAR MEDIA YADHAMINI LIKI YA KIKAPU MKOA WA DAR ES SALAA
02/ 08// 2017

CHAMA Cha  Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA ) leo  kimemtambulisha  mdhamini  wa Ligi yake inayoendelea  ambaye ni Kampuni ya Star Media  atakaye dhamini gharama  zote  za uendeshaji wa Ligi hiyo inayoelekea ukingoni.

Akizungumza  katika mkutano na waandishi wa habari Mwenyekiti wa BD  Bwana  Ukeri Onesmo  mesema  wamefurahishwa na  udhamini  huo huku wakiwa na imani kwamba utaleta hamasa kwa wachezaji kwa ujumla.

Amesema  hivi sasa  BD wameweka mikakati ya  kuendesha  mchezo huo  kibiashara kwa kushurikiana na Taasisi mbalimbali huku lengo kuu likiwa kurudisha hadhi ya mchezo huo iliyopotea.

Ligi hiyo inatarajiwa kuingia kwenye hatua ya  mtoano  huku timu zitakazotinga  hatua ya fainali  itakayorindima Agosti 9   Mwaka huu Uwanja wa Ndani wa Taifa.No comments:

 
 
Blogger Templates