Social Icons

Wednesday, August 9, 2017

MGOMBEA KITI CHA URAIS TFF SHIJA RICHARD SHIJA AANIKA MIKAKATI YAKE


MGOMBEA wa nafasi ya Urais Shija Richard Shija mwenye shati jeupe na tai ya bluu, anayefuata kuli ni  Mwanahabari Muandamizi wa Kituo cha Azam TV na kutoka kushoto ni Mwanahabari kutoka gazeti la Nipashe Faustine Felicine na Khadija Kalili wa ITV ,Radio One jana Agosti 8 mwaka huu alianza  kampeni zake huku akitanabaisha mikakati yake endapo atafanikiwa kuingia madarakani .

Shija alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari  amesema soka ndiyo mchezo unaokusanya wapenzi wengi kuliko mchezo wowote nchini na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla na wadhamini wengi wangependa kutumia fursa hii kuwafikia wadau wao.
Alisema endapo ataingia madarakani ataweka mfumo rasmi wa kuendesha soka ili wadhamini waweze kuvutiwa kufanya uwekezaji katika soka.

Amesema akiwa madarakani ataanzisha kampeni ya kutoa elimu ya kutosha na kutoa kushawishi kwa wazazi kuwekeza na kuruhusu watoto wao wenye vipaji waingie kwenye michezo kwani ukweli ni kwamba mtoto mwenye kipaji anaweza kupata mafanikio katika maisha kwani kichezo inalipa kuliko kazi nyingine za kuajiriwa.

 Aidha amesema kuwa katika utendaji wake atahakikisha familia ya kichezo inaendeshwa kwa uadilufu na kuheshimu uhuru na mipaka ya kitaasisi bila kuingiliana kimaamuzi huku akisisitiza kuwa katika uongozi wake hautavumilia vitendo vya aina yoyote vya rushwa na ufisadi.

No comments:

 
 
Blogger Templates