Social Icons

Monday, July 24, 2017

WAZIRI MAGHEMBE APOKEA MABILIONEA 28 SERENGETI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi.

Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.
................................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa  Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

Mabilionea hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda, Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.

Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,  Prof. Maghembe aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores) na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti". 

Prof. Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye  amani na vivutio vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

(SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM)

No comments:

 
 
Blogger Templates