Social Icons

Tuesday, May 30, 2017

UNESCO, GPF WAWAJENGEA UWEZO CHUO CHA MWL. NYERERE

Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere  na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Vijana kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nelson akieleza namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha amani katika Jamii.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi   Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
 Mwakilishi kutoka Raleigh Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia pia alielezea fursa zinazotokana na kujitolea
Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship'  zinazotolewa sehemu mbalimbali, na kuwasihi kuwa wasikate tamaa kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kusoma nje ya nchi.
 Charles Ndiku akiwaelekeza vijana namna mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia kupata ajira,na aliwasisitiza ili waweze ishi kwa amani yawapasa kuishi maisha bora ikiwa ni pamoja na kuwa na kipato endelevu.
Mwenyekiti wa programu kutoka Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam William Peter akieleza namna vijana wanavyoweza kubadili mitazamo na kuwa na mawazo chanya ya maendeleo
 Vijana mbalimbali wakichukua yale yaliyokuwa ya Muhimu
 Vijana wakiwa wananyoosha mikono ishara ya kuonesha kuwa wameelewa vizuri kwa yale yote waliyoyasikiliza
 Vijana wakiwa wanasikiliza kwa Makini.
Semina ikiendelea
Picha ya Pamoja
Picha zote na Fredy Njeje

"Kiongozi bora ni pamoja na yule ambaye anahakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na watu anaowaongoza" hayo yalisemwa na bwana Nelson aliyekuwa mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nchini Tanzania  wakati wa semina ya vijana katika kushiriki programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania. 

Alisema kuwa kiongozi makini ni yule anayehakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na kuwafanya wafanyakazi wake waishi kama familia moja ili kuondoa migogoro mbalimbali ambayo inaweza ikazuirika.

"Amani inatakiwa kudumishwa kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla" alisema Nelson na kuongeza kukosekana kwa amani kunaweza kusababisha  maafa kama vifo kwa sababu ya vita pia uchumi kuyumba kutokana na watu kuhofia kufanya shughuli za kimaendeleo kwa sababu ya machafuko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.

Nae  Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili ‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.

Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao

Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya vijana 180, kutoka vyuo vikuu vya Mwalimu Nyerere,CBE, TIA, Bagamoyo, Kampala International University  na St. Joseph, wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana .

No comments:

 
 
Blogger Templates