Social Icons

Saturday, May 27, 2017

RC MAKONDA AKABIDHIWA MWENGE WA UHURU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo  John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo  James Mkumbo wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi wakijadili jambo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya UbungoJohn Lipesi Kayombo (Kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  Kisare Makori (Kulia) wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com  Mathias Canal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Muonekano wa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam ukitokea Mkoani Lindi.
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Me 27, 2017 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

Mara baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni Tarehe 28/05/2017, Siku ya Tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, Tarehe 30/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na Tarehe 31/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mhe Makonda alisema kuwa Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa kuwa Jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa.

Rc Makonda amebainisha kuwa jumla ya Miradi 40 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa na  thamani ya Shilingi Bilioni 244,392,530,334 ambapo Miradi 12 itazinduliwa, Miradi 15 itawekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili itafunguliwa na Miradi 11 itatembelewa.

Mhe Makonda amewapongeza wananchi wa Mkoa wa  Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili huku akitoa wito kwa Wakazi wa Manispaa ya Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote utakapozuru kwani pamoja na mambo yote Mwenge wa Uhuru ni urithi na nembo ya umoja katika maendeleo yetu.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa weledi wake katika utendaji hususani katika kudumisha amani na kuchagiza ukuzaji wa uchumi wa nchi kwa kutilia msisitizo uwajibikaji serikalini, Kukemea wizi na Ubadhilifu wa Mali za umma sambamba na Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

Mhe Zambi alisema kuwa Wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli katika mapambano dhidi ya wizi wa Mali za Watanzania hususani Vita  ya kiuchumi aliyoianza hivi karibuni kwa kuzuia Mchanga wa dhahabu kusafirishwa kwenda nje ya nchi. 

Mhe Zambi ametoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake mkoani Dar es salaam siku ya tarehe 31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani siku ya tarehe 01/06/2017 katika Uwanja wa kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kuelekea Mafia .

No comments:

 
 
Blogger Templates