Social Icons

Monday, May 8, 2017

MAELFU WAJITOKEZAZA IBADA YA MSIBA MKUBWA ULIOLIKUMBA TAIFA

 Miili ikiwa imebebwa na magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

 Picha za wanafunzi 32 ambao wamefariki kwenye ajali iliyotokea Karatu Jumamosi Mei 6 mwaka huu.
 Umati wa wakazi wa Jiji  la Arusha na mikoa ya jirani waliojitokeza kuaga miili ya watoto hao.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameomba vyombo vya usafiri kubeba abiria kulingana na uwezo wa chombo cha kusafiria.Suluhu aliyasema hayo leo kwenye hafla ya ibada ya mazishi ya miili ya wanafunzi waliofariki Jumamosi Mei 6 mwaka huu kwenye ajali iliyotokea  Karatu Mkoani Arusha.

Suluhu amekazia suala la kuwa makini kwenye vyombo vya usafiri kua makini katika kuahkikisha sheria za usalama barabarani zinazingatiwa  ipasavyo.


Ajali hii i emegusa mioyo ya kila mtanzania ,msiba huu umetupa majonzi mengi huku ukithibitishwa na wingi wenu ambao mmejitokeza. Mungu azilaze pema roho hizi za watoto wetu. Innalillah wainna ilaihRajiun bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.


"Msiba huu umeitingisha Afrika Mashariki  na kati, maisha yetu siyo mengi siku zetu ni chache  hapa duniani Mwenyeezi Mungu amechukua hizi roho,  nchi yetu imekunywa damu nyingi, mungu tunakuomba ukawasaidie madereva ili waweze kuepusha ajali na serikali ikasimamie suala zima za usafiri wenye usalama".
Hayo yalisemwa na Askofu Mwizarubi wa Kanisa la EAGC.

Aidha alisema kuwa kila mwanadamu ana mambo yake ya siri ambayo hutopenda mtu mwingine ayafahamu ana anayejua ni Mwenyeezi Mungu peke yake.

Huku akisema kuwa hakuna mwanadamu anayeijua kesho,"Wenzetu walipanga wakaenda na laiti kama wangelijua hili wasingeenda safari yao  naamini ndugu zetu hawa wamemaliza safari yako kwa amani naamini hivyo sisi tulio hai ndiyo tunapaswa kujifikiria nafsi zetu".

Shughuli hiyo imehudhuriwa na  viongozi mbalimbali akiwemo Kiongozi wa Kambi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendelo CHADEMA pia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako. Waziri wa Elimu wa Kenya

No comments:

 
 
Blogger Templates