Social Icons

Wednesday, April 5, 2017

UCHAGUZITAFCA KINONDONI MEI 7

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni unatarajiwa kufanyika Mei 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Tarehe ya uchaguzi huo imetangazwa na Kamati ya Utendaji ya TAFCA Kinondoni inayomaliza muda wake iliyokutana Jumapili, Aprili 2 mwaka huu chini ya Mwenyekiti Eliutery Mholery (0715 621 667) na Katibu Mkuu wake Mbwana Makata (0655 520 129).

Fomu kwa ajili ya wagombea zimeanza kutolewa Jumatatu, Aprili 3 mwaka huu kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA).

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ni Ijumaa, Aprili 7 mwaka huu.

Ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA ni sh. 50,000 wakati Mhazini, Mhazini Msaidizi na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni sh. 30,000. Ajenda ya uchaguzi itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Kawaida ambao mbali ya taarifa ya utendaji, Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake pia itawasilisha ripoti ya mapato na matumizi.

Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA Kinondoni inaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa TAFCA, Ramadhan Mambosasa.

IMETOLEWA NA TAFCA KINONDONI

No comments:

 
 
Blogger Templates