Social Icons

Monday, February 27, 2017

ASHINDA GARI DROO YA ENHANCE AUTO TANZANIA LIMITED


Mstahiki Meya wa Kinondoni , Banjamin Sitta, jana alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla droo ya kwanza  ya  Kampuni ya magari Enhance Auto Tanzania na Kampuni mama Enhance Auto Japan.

Hafla hiyoo iliandaliawa kwa minajili ya kutoa zawadi kwa wateja wao   zaidi ya watu 6,000,000 walishiriki kwenye usaili wa kutumia mtandao wa “enhance-auto.jp”  .
Kwenye  droo hiyo Dovick Moria  alishinda gari aina ya Noah toleo la 2002. Madhumuni ya shindamo hilo ni kuhamasisha watanzania wengi kutumia mtandao wa enhance-auto.jp ili kuleta tija la kibiashara.

Meneja wa Enhance  Auto Tanzania Limited   Aatif Butt  alisema  kuwa biashara ya magari kwenye mtandao ( online trading) inakua kwa haraka sana hapa nchini Tanzania.
Inawapa wateja nafasi ya kununua gari lenye ubora na chaguo la uhakika.
Aidha Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamin  Sitta aliwashauri watanzania kutumia fursa  ya biashara ya kwenye mtandao (online business) ilikuchochea ukuaji wa biashara hapa  nchini Tanzania.

Mstahiki Meya Sitta aliwapongeza wanao tumia APPS kutambulisha biashara zao na kwa mauzo pia.

Enhance Auto Tanzania na Kampuni mama Enhance Auto Japan, wanatoa fursa kwa walio mikoani kutumia himaya yao kununua magari kwani wanao mfumo mzima wa Clearing and forwarding.

Kamouni hiyo  pia wanatoa magari bandarini  kwa ufanisi wa hali ya juu dp na kutoa waranti ya mwezi mmoja ambapo kitu chochote kikipotea kwenye gari itakuwa jukumu lao kulipa. 

Mbali ya Meya  pia alikuwepo DAS wa Kinondoni Gift Msuya ambaye alitoa pongezi zake kwa mshindi.

No comments:

 
 
Blogger Templates