Social Icons

Thursday, January 5, 2017

DKT SENKORO KUZIKWA JUMAMOSI MAKABURI YA KINONDONI

Na Frank Shija - MAELEZO

Mwili wa aliyekuwa Mgombea wa kwanza Mwanamke kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Anna Senkoro unatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi tarehe 07/01/2017 kuanzia saa 8:00 mchana.

Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Bwana. Fred Sendim ambaye ni Msemaji wa Familia ya marehemu Dkt. Senkoro.

“Mipango ya mazishi inaendelea vizuri nyumbani kwake Segerea, pia nitumia fursa hii kutoa shukrani za kipekee kwa wote wanaoendelea kutufariji na kushirikiana nasi bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.”

Alisema Sendim. Msemaji huyo wa familia amesema kuwa taratibu za mazishi zitataunguliwa na Ibada maalum itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho kuanzia saa Saba mchana katika Kanisa la Winners lililopo Banana, Ukonga jirani na Kituo cha Mafuta cha Oil Com.

Awali akielezea kifo chake msemaji wa familia hiyo amesema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambapo juzi tarehe 04 majira ya saa 11 alfajiri alizidiwa na kupelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na baadaye alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alifikwa na mauti mnamo saa 3:30 asubuhi.

Dr.Anna Senkoro alikuwa mgombea wa kwanza mwanamke kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kupitia Chama cha APPT Maendeleo, Marehemu ameacha watoto wa tatu na wajukuu wa wiwili. Mungu hailaze roho ya Maerehemu mahali pema peponi amina.

No comments:

 
 
Blogger Templates