Social Icons

Monday, December 26, 2016

RAIS WA TFF JAMAL MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA BUKUKUWakati mwili wa Mwanahabari, Mpoki Bukuku ukiagwa leo jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga kutokana na kifo hicho.

Mpoki Bukuku alifariki dunia Ijumaa iliyopita, alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kugongwa na gari eneo la ITV Barabara ya Bagamoyo jijini.
Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda  Mkoani Dodoma  kwa ajili ya mazishi.

No comments:

 
 
Blogger Templates