Social Icons

Monday, December 19, 2016

MKURUGENZI WA JAMII FORUM APATA DHAMANA

Mkurugenzi  wa Jamii Forum  Maxence Melo   pichani  juu amepata dhamana leo baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa  na wadhamini wawili  huku kila  mmoja alisaini dhamana ya maneno   ya Sh.Mil.5 na kuachiwa huru  na Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam Godfrey  Mwampamba.

Melo alishikiliwa na Polisi zaidi ya saa 72 kabla ya kupandishwa Mahakamani  Ijumaa Desemba 16 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na  makosa manne likiwemo  la kuzuia  upelelezi wa polisi.Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 29 mwaka huu.No comments:

 
 
Blogger Templates