Social Icons

Sunday, October 9, 2016

MAMIA YA WAKAZI WA MKOA WA DODOMA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA MAMA SALOME KIWAYA

Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma leo   wamejitokeza  katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoani humo Salome Kiwaya.

Marehemu alifariki juzi baada ya ajali ya gari mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda nyumbani kwao Njombe  ambako ndiko mazishi yatafanyika.

Mama  Kiwaya atakumbukwa  kwa mchango wake wa kujitoa kwa hali na mali katika shughuli mbalimbali mkoani Dodoma

Kabla ya kuingia kwenye ulingo wa Siasa alikuwa mmfanya kazi wa Ustawishaji Makao Makuu CDA, pia  yeye ndiye alikuwa  Mratibu wa kwanza  shindano la urembo  la Miss Dodoma huku akifanikiwa  na kumtoa aliyekuwa  Miss Tanzania Emily Adolf 1995.
Mbali na urembo pia  alikuwa ni mmiliki wa bendi pekee  Mkoani  Dodoma iliyofahamika  kwa  jina la SAKISTARS.
Pichani juu  marehemu mama Salome  Kiwaya enzi za uhai wake.

Blog hii inaungana na wote katika msiba huu bwana alitoa na  bwana ametwaa jina lakelihimidiwe.

No comments:

 
 
Blogger Templates